
TANZANIA YOUTH SHINNING ORGANIZATION
K |
uhusu – TAYOSO:
TAYOSO ni jumuiya ya wasomi Tanzania kuanzia sekondari “A- Level” mpaka chuo, yenye kuleta mtandao wenye tija kwa wanachama na Taifa kwa ujumla, katika misingi ya upendo, uzalendo, amani na ushirika baina ya wanachama na ambao si wanachama.
Jumuiya imeweza na inatarajia kupata wanachama wengi kutokana na misingi bora ya upendo, uzalendo, amani na ushirika iliyojiwekea ambayo imevutia watu wengi kuwa tayari kudumisha na kuendeleza misingi hiyo katika jamii zao husika kwa umoja.
Maono ya TAYOSO:
Kuwa na jamii ya kisomi iliyoendelea kimwili na kimawazo chini ya misingi ya upendo, uzalendo, amani na ushirika sehemu yoyote ilipo.
Malengo ya TAYOSO:
- Kuwezesha na kutoa elimu ya kimatendo na nadharia katika kutambua umuhimu wa kuishi kwa umoja na ushirika baina ya mtu na mtu na jamii kwa ujumla.
- Kuwezesha wanachama kujifunza jinsi ya kupokea tamaduni za kigeni katika hali isiyoleta mkanganyiko wa maadili na umoja wa kitaifa.
- Kutengeneza njia za kuwezesha katika mahitaji mbalimbali ya kimaisha baina ya wanachama na koutoa matabaka.
- Kukumbusha umuhimu wa kujilinda kimwili dhidi ya maradhi na kifikra dhidi ya mawazo yasiyojenga jamii imara katika nyanja zote kutambua mabaya na kuyakwepa.

Matarajio ya TAYOSO:
Kuwa na wanachama katika kila chuo na sekondari wanaokuwa katika misingi iliyowekwa na taasisi na yenye ushindani katika kusoma kwa bidii na mambo yote yenye mafanikio.
FAIDA YA KUWA MWANACHAMA WA TAYOSO:
- Kuwa ndani ya ushirika wenye tija sehemu wanachama walipo katika kusoma pamoja na kusaidiana.
- Kuwa karibu na waajiri au viongozi wa juu wa Taasisi mbalimbali binafsi na za kiserikali ambao TAYOSO itawaomba katika kutoa mada, kusaidia nafasi za “field” elimu kwa vitendo ajira za muda na za kudumu katika taasisi zao na kupata mtandao imara hapo baadae.
- TAYOSO itasaidia endapo mwanachama amepata matatizo asiyoyatarajia na kudhoofisha hali yake kimasomo na kimaisha mfano kiafya au kufiwa na wazazi au walezi waliokuwa tegemeo lake au kuibiwa sehemu kubwa ya mali zake, kulingana na hali ya bajeti.
- TAYOSO itatoa vyeti vya uanachama ambavyo vitaongeza sifa kwa mwanachama kwa shughuli yoyote ya kijamii na taasisi.
- Taasisi itatoa ajira kwa nafasi zitakazopatikana ndani ya taasisi ambazo zitahitaji wafanyakazi ikizingatia juhudi na sifa za wanachama katika kufata misingi iliyowekwa na taasisi.
- Kwa wanachama waliopo zaidi ya miaka mitatu taasisi itasaidia endapo mwanachama ataoa au kuolewa kutokana na bajeti itakavyo ruhusu.
Kukutana TAYOSO:
Bonaza zitaandaliwa kwa wanachama katika vyuo husika na taasisi.
Kumb; Ikiwa kuna wanachama zaidi ya chuo kimoja sehemu moja kwa mfano Dodoma Bonanza litajumuisha wanachama wa vyuo vyote pamoja watashiriki katika michezo mbalimbali kama jinsi watakavyojiandaa na kuifanya sherehe ya pamoja kuzawadia washindi na kutoa mada fupi kwa kufuata malengo kama yalivyoandikwa hapo mwanzo Hii itakuwa siku maalumu kwa wanachama kupendeza” THE GREAT SHINNING DAY” na kufurahi pamoja.
“GHARAMA ZOTE ZITATOLEWA NA TAASISI”
THE GREAT SHINNING DAY ITAKUWA MARA MOJA KWA KILA SEMISTA AU MUHULA WA MASOMO KWA SEHEMU HUSIKA.
Habari TAYOSO:
- Kutaandaliwa magazine zilizojaa habari za wanachama na matukio mbalimbali yatakayo kuwa yakiendelea ndani ya taasisi magazine hizi pia zitakuwa na matangazo ya wadhamini mbalimbali.
- Tayari imeandaliwa blog ambayo kama magazine ilivyo nayo itatoa habari mbalimbali na matukio pamoja na kuonyesha matangazo ya wadhamini.
- Tuko mbioni kuandaa kipindi katika Television ambacho kitaitwa “TANZANIA GREAT SHINNING DAY” Kikionyesha matukio mbalimbali ya vijana wa “YOUTH SHINNING” kama kitakavyo buniwa nacho kitaonyesha pia matangazo ya wadhamini.
- Habari na maelezo mbalimbali pia yatasambazwa kupitia simu za mkononi za wanachama na kwenye e mail zao.
JINSI YA KUWA MWANACHAMA:
- Mwanafunzi yeyote wa chuo au wa sekondari A- Level pasipo kujali umri, jinsia, rangi, asili ama taaluma anayosomea.
- Ada ya uanachama kwa semester moja au muhula mmoja Tsh5,000/= kwa kila mwanachama anaweza kulipa Tsh 10,000/= kwa mwaka mzima.
- Kutakuwa na “Coordinators kwa kila chuo ambao watahusika na kusimamia shughuli zote za uanachama na wanachama kwa sehemu husika kwa uaminifu mkubwa.
MAHITAJI YA TAYOSO KWA MWANACHAMA:
- Mwanachama kuwa tayari kusimamia katika misingi iliyowekwa na taasisi.
- Kutoa ushirikiano kwa wadhamini mfano ukiwa kampuni ya simu inatudhamini kila mwanachama ataombwa kuwa na line ya mtandao husika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja mwazo wa muhula wa masomo nazo zitatumika kama njia kupashana habari ndani ya taasisi au ikiwa ni taasisi ya fedha mfano benki wanachama wanaombwa kuwa na a/c katika benki hiyo ndani ya semester au muhula mmoja wa masomo navyo vitadumu katika kipindi chote cha udhamini.
Hii ni kuongeza nguvu ya wadhamini kutudhamini kwakuwa ada ya uanachama peke yake haiwezi kuendesha shughuli nzima za taasisi.
- Moyo wa kizalendo , upendo na ushirika katika jamii inayozunguka mwanachama na taifa kwa ujumla katika misingi ya utii.
VYANZO VYA MAPATO:
- Ada za wanachama
- Wadhamini
- Misaada toka sehemu mbalimbali
JINSI YA KUDHAMINI TAYOSO:
- Ili kutoa nafasi nzuri kwa taasisi, shirika au kampuni kufaidika na udhamini, taasisi imetaka mdhamini asiwe yule anaefanya aina moja ya shughuli au biashara na kampuni nyingine.
- Kampuni shirika au taasisi husika itatudhamini pale itakapokubali maombi ya TAYOSO yatakayo tumwa katika sehemu husika kulingana na maombi.
- Udhamini uwe wa miezi sita au mwaka kutokana ridhaa ya mdhamini
FAIDA KWA KAMPUNI KUTOKANA NA UDHAMINI:
- Wanachama kuwa namoyo wa kizalendo na kampuni mfano:
Ikiwa ni kampuni ya mawasiliano – wanachama wote ndani ya mwezi wa kwanza wa muhula au semester wataombwa kuwa na line za mtandao husika nazo zitatumika kama mojawapo ya njia za mawasiliano ndani ya taasisi
Ikiwa ni taasisi ya fedha mfano benki:
Wanachama wataombwa kujitahidi kuwa na a/c ndani ya muhula mmoja au semister moja ya mwaka wa masomo baada ya udhamini kuanza.
Hiyo juu ni mifano tu, yaweza kuwa hoteli au kampuni yeyote. Makubaliano yote yataendelea kusisitizwa kwa wanachama kwa kipindi chote cha udhamini.

- Matangazo ya wadhamini yatakuwa yakionekana kwenya jarida litakaloandika habari na matukio mbalimbali ya taasisi.
- Matangazo ya wadhamini yataonekana pia kwenye blog ya taasisi ambayo itakuwa wakati wote kutoa habari na matukio ya taasisi na ratiba mbalimbali.
- Nembo za wadhamini zitaonekana katika mabango mbalimbali, T- shirt na magari yatakayotumiwa na taasisi katika shughuli mbalimbali.
- Matangazo ya udhamini pia yatakuwepo katika shughuli za michezo yaani Bonaza zitakazo wakutanisha wanachama katika sehemu zao yatakayofanyikamaramoja kwa kila semister au muhula wa masomo
Kwa kufanya haya yote tunatarajia kwa uzalendo sehemu kubwa ya wanachama kama si wote kuwa wateja wa karibu kwa bidhaa za kampuni zote zitakazotudhamini kwa kipindi chote cha udhamini na kuandaa wateja wengi wa hapo baadae.
MATUMIZI TAYOSO:
- Gharama za kulipa wafanya kazi wa TAYOSO Managing Director na Assistance General Secretary, coordinators, Accountant, lawyer na wengine.
- Gharama za kuandaa Bonanza kwa wanachama katika sehemu zao husika.
- Gharama za usafiri na ni mpango wetu kuwa na basi dogo japo mbili bajeti ikiruhusu ili kuendesha shughuli mbalimbali za taasisi kwa wanachama wake.
- Gharama za mavazi maalumu mfano T- Shirt zilizoprintiwa nembo ya taasisi na wadhamini.
- Gharama za kulipa watoa mada.
- Gharama zilizokadiriwa kusaidia matatizo mbalimbali yatakayojitokeza kwa mwanachama kama ilivyoelezwa kwenye faida ya kuwa mwanachama hapo mwanzo.
- Gharama za media kuprinti magazine, communication, stationeries na mengineyo katika kuendesha taasisi.
- Gharama za kuandaa mahala pa ofisi na vifaa.
Ofisi itaanza sehemu moja kama pendekezo la kufungua ofisi kuu na baadae katika sehemu tofauti, kama bajeti itavyoruhusu kwa makubaliano ya wanachama na uongozi.
VITU VITAVYOMTOA MWANACHAMA NJE YA TAYOSO:
- Kutofuata misingi iliyowekwa na taasisi ya upendo, uzalendo, amani na ushirika kwa makusudi pasipo kujirudi badala ya kuonywa
- Kuwa mfano ambao si mzuri kwa jamii baada ya kufanya kitendo kiovu mfano kuiba, kutenda kosa la jinai, ugomvi na mengineyo yanayoendana na hayo.
- Kuwa mtu wa matabaka na mengine sawa na hayo.
- Kuwa mshabiki wa maovu yanayovuruga amani kwa jamii na moyo wa kizalendo kwa taifa.
- Kudanganya kwa njia yoyote kwa manufaa binafsi ndani au nje ya taasisi.